Mada

111 - Balehe

Kati ya miaka 10-14 wasichana na wavulana huanza kuona mabadiliko katika miili yao, ya kimili na kihisia, na huchukua miaka kadhaa, mabadiliko haya huitwa balehe, msichana huanza kuzalisha mayai ya uzazi, mwili hupevuka na kujenga uwezo wa kupata watoto, lakini haimaanishi kwamba huu ni wakati mwafaka wa kupata mtoto, maziwa huanza kukua, nyonga hutanuka na nywele huota sehemu za siri na makwapani.

112 - Mzunguko wa mwezi

Wakati wa hedhi, kuta za mfuko wa kizazi(uterasi) hubomoka na kutoka nje pamoja na damu kupitia uke, hutokea kila mwezi ndani ya siku nne hadi saba, jambo kama hili ni kawaida na hutokea kila mwezi.Tangu kuingia kwenye siku zako(damu inapoanza kutoka) mpaka siku unayoingia tena kwa kawaida ni siku 28, huo ndio mzunguko japo wengine huchukua muda mrefu zaidi. Wegine hawasikii maumivu wakati wa hedhi, wakati baadhi wakipata maumivu makali, kama unahitaji kubadili pedi au vitambaa zaidi ya mara nne, omba ushauri wa mkubwa wako ama daktari.

113 - Mimba

Baada ya kuvunja ungo msichana hupata hedhi mara moja kila mwezi, siku ya kwanza ya hedhi ni siku yakwanza ya mzunguko, baada ya damu kutoka, yai moja linaanza kukua ndani ya kokwa, vilevile utando wa damu ndani ya mfuko wa uzazi huanza kujengeka ili ukaribishe mimba, ndani ya siku 11-14 yai hupevuka ndani ya kokwa na halafu husafiri kwenye mrija wa kupitisha mayai hadi mfuko wa uzazi, mwanamke anapata mimba kama yai litaungana na mbegu ya kiume, ina maana kama msichana akikutana na mvulana wakati yai linakaribia au limekwisha pevuka atapata ujauzito.

114 - Magonjwa

Magonjwa haya huleta maumivu makali na hata wakati mwingine kifo, baadhi ya magonjwa hayo ni pamoja na UKIMWI, kisonono, kaswende, klamdia na kadhalika, dalili zake huwa kuwashwa sehemu za siri, vidonda sehemu za siri na kwa wanawake huweza kuhisi maumivu makali chini ya tumbo , njia kuu ya kujiepusha na magonjwa hayo ni kuacha kujamiiana hadi pale utakapoolewa, na itakapofikia muda huo kuwa mwaminifu kwa mwenza wako.

114 - Mimba za utotoni

Wataalamu wanashauri msichana anastahili kubeba mimba akiwa na zaidi ya umri wa miaka 20, kabla ya umri huu, mwili wa msichana bado haujakomaa vizuri, viungo vya uzazi bado ni vidogo na ngozi ni laini, vilevile mfupa wa nyonga vado ni mwembamba kiasi cha kumwezesha mtoto kupita wakati wa kuzaliwa.

Matatizo wanayokutana nayo ni pamoja na mapigo ya moyo kuwa juu, kukwama kwa mtoto, upasuaji wakati wa kujifungua, kujifungua kabla ya wakati na watoto kuzaliwa njiti.

Athari nyingine ni kukatisha masomo, hali duni kiuchumi na wakti mwingine kutengwa katika jamii.